Tutazidi kuwaambia wananchi wetu wajue thamani ya miundombinu ya reli ya treni ya umeme (SGR) hii na faida zake na kwamba hii ni mali yao na wao ndio wawe walinzi wa kwanza kuhakikisha kwamba miundombinu inakuwa ni ya faida na kutunzwa.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 miradi mipya ya uwekezaji 630 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.68 inayotekelezwa na makampuni ya India imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).